Ilikuwa kwenye mechi iliyo endeshwa hii jumapili tarehe 21 Aprilia kwenye uwanja wa kadutu katika michuwano ya ligi ya kandanda jimboni Kivu kusini Lifski.

Timu la Ruzizi ikaweza kuiharibi vikali Fc Renaissance kutoka Kabare, Ruzizi ikaweza kujifariji kisha kupoteza mechi ya pili ambayo iliwezakuwa kutanisha na Timu ya TP Espoir ya huko Kalonge.

Ruzizi iliweza kufaulu kuishinda Fc Renaissance ilikuwa mukipindi ya pili ya lala Salama sahabu kipindi ya kwanza ilikuwa ya 0-0 pande zote mbili.

Timu ya Ruzizi ikafaulu kuja Goli lake la kwanza ilikuwa munamo dakika 65′

Na goli la pili iliweza kuingiya mu dakika za 67′

Na goli ya tatu ikaingiya munamo dakika ya 71′, kupitiya hii ushindi Timu ya Ruzizi ikachukuwa na fasi ya pili katika Kundi lake na pointi sita 6pts kwa mechi tatu 3-0

Tuseme kwamba mwahii Kundi ya Ruzizi ni TP Espoir inakuwa ikichukuwa nafasi ya kwanza ikikuwa na pointi 6pts Ila haija poteza mechi yeyote ile.

Ila kabla mechi ya Ruzizi na Renaissance palikuwa piya mechi ya Kati ya Fc Kenge na Cs Bande rouge , na Timu ya Fc Kenge ikaweza kushindwa mbele ya Bande rouge kwa Goli moja zidi ya Tatu 1-3.

Piya Ushindi huo umepatiya Bande rouge kitumaini ya kuendelea shikiliya na fasi ya kwanza katika Kundi lake na pointi 9 pts Ku mechi tatu ambayo imesha cheza, Bande rouge inakuwa ikisubiriya mechi yake ya mwisho ambayo itakuwa ikicheza na As La victoire kutoka Kavumu.

Michuwano itakuwa ikiendelea hii jumatatu tariki 22 Aprilia kwenye uwanja wa kadutu ni mechi mbili zitakuwa kwenye mpango.

Pa saa 13h As Umoja itakuwa inaipokea Fc Umoja.

Napa saa 15h Lubunga académie itakuwa ikipima maji naunga na Oc Gorille.

Patrigal Basimarha Tonton.

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *