Timu la Oc Gorille imekanyagwa vikali na Fc Immortel kwa goli tatu kwa sufuri (3-0). Ilikuwa  kwenye mechi iliyo endeshwa hii jumamosi tarehe 20 april kwenye uwanja wa Kadutu katika michuwano ya ligi ya jimbo Kivu-Kusini.

Tuseme kwamba ni maraba ya kwanza hizi timu mbili zinaingiya kwenye michuwano ya ligi ya kandanda jimboni Kivu-Kusini.

Oc Gorille ni timu la wambuti kutoka kahuzi Biega ambawo wamejitahidi kuingiya mara yao ya kwanza kwenye hii michuwano.

Lakini wakati hili timu iko ikicheza mechi hawafanani kama ni timu la wambuti kimchezo ambayo wakuna wakionesha kwenye uwanja. Timu hili liko likijitahidi kucheza sana wanapokuwa uwanjani ingawa ni wambuti, ila njisi inavyoonekana tuseme ya kwamba wanahitaji msaada kupitiya usapoti na kuwaunga mkono kwa ngazi zote.

Piya tuseme ya kwamba hii michuwano itakuwa ikiendelea hii jumapili tariki 21 april. Na ni mechi mbili zitakuwa kwenye mpango kwenye uwanja wa Kamituga.

Pa saa saba (13h) Ac Vijana itakuwa ikipokea Fc Bisonnga.

Na paa kenda (15h) Fc Renaissance itakuwa ikipima maji na unga na As Ruzizi.

Patrigal Basimarha Soka

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *