LIFSKI 2024  : As KASMS imeteteya Fc MALWA , ED MBILA ikatolewa na MUNYAGO FA.

Ilikuwa kwenye mashindano ya Jimbo la Kivu kusini kwenye raundi ya nane iliyo endeshwa hii jumatano tarehe 29 may kwenye uwanja wa Concorde mtaani Kadutu.

As KASMS imejipatiya tiketi ya kuingiya kwenye robo fainali Kisha hii ushindi mnono ambao wameupata mbele ya FC KATANGA SPORT kwakuilaza Timu ya FC KATANGA SPORT kwa goli mbili kwa ziro 2-0, AS KASMS imekuja kuteteya Mwenga na Kamituga Kisha kutolewa kwa Timu ya ED MBILA kwa mikwaju ya pelnati na MUNYAGO FA ya Uvira.

AS KASMS wamekuja uwanjani na hasira kali ya kujiteteya na kuteteya wilaya yote ya Mwenga na Kamituga tuseme kwamba hapo mbele ni Timu ya Fizi ya FC CAFÉ DU CONGO iliweza kuitowa AS KASMS Kupitiya mikwaju Ya pelnati, KASMS Haiku kukubali iweze kuachiya na Fasi FC KATANGA SPORT kupitiya Ujasiri ambao wamekuja Nayo.

Hii timu ya FC KATANGA SPORT ingawa vitisho ambayo ilikuwa Nayo haikuzuwiya wasi teketezwe na KASMS ya Kamituga, tueleze ya kwamba KASMS iliweza kujaza goli lao la kwanza ilikuwa mu dakika ya 32′ ya kipindi ya kwanza na goli la pili likaweza kuingizwa munamo dakika 60′ mukipindi Ya lala Salama matokeo rasmi ilikuwa ya 2-0 kwa faida ya KASMS natayari imeingiya kwenye boro Fainali.

Ila kabla ya hii mechi palikuwa na ambao ilikuwa nakutanisha timu ya ED MBILA yake  Mulungula Mukamba Jean fort ambayo ilikuwa inaipokea MUNYAGO FA . Na Timu ya ED MBILA ikaweza kutolewa kupitiya mikwaju ya pelnati na MUNYAGO FA ingawa Bahati nyingi ambazo Timu ya ED MBILA iliweza kuzipata munamo dakika 90′ za mchezo ila haikuwa na Bahati ya kufungali .

ED MBILA ni pekee ya Kamituga iliweza kuondoshwa bila Kupoteza Mudakika 90′ ila ni mikwaju ya pelnati ndiyo wameweza kuwatowa Kisha dakika 90′, MBILA iliweza Kupoteza Kwa 1-4 kwamikwaju ya pelnati hadi Sasa Kamituga inakuwa ikiwakilishwa na Timu Moja nani Timu la KASMS kwenye robo fainali.

Patrigal Basimarha soka.

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *