LIFSKI 2024 : Ac Rangers na TP Mobale zime jikatiya nauli ya kuingiya kwenye raundi ya nanne.
Yote imefanyika kwenye mechi mbili ya Fainali Ndogo zilizo chezeka hii jumamo tarehe 18 may kwenye uwanja wa concorde mtaani Kadutu.
Kwenye mechi ya 13h Ac Rangers imejipatiya ushindi zidi ya FC Lungwe ya Burhinyi kupitiya mikwaju za pelnati, ilikuwa Kisha kwenda Sare ya 1-1 pande zote katika dakika makuki Kenda za mchezo kwa umarufu 90′.
Tuseme kwamba FC Lungwe ilikuwa ya kwanza kujaza goli ilikuwa mu 10′ za mchezo piya AC Rangers ikakuja kugombowa munamo 17′ ni matokeyo ambayo iliweza kumaliza kipindi ya kwanza.
Mukipindi Cha lala Salama Ama kipindi cha pili hakuna Timu iliweza kufunga goli Ama kufungiwa matokeyo ilikuwa Yale Yale ya 1-1 pande zote.
Lakini kwenye mikwaju ya pelnati timu ya Ac Rangers ikajipatiya ushindi kwakuishinda Fc Lungwe kwa mikwaju 4-2, Rangers inakuwa Timu ya kwanza ambao inajikatiya nauli ya hapa mjini Bukavu.
Piya palikuwa na mechi ya pili Kati ya TP Mobale yaKamituga na Munyago FA ya Uvira.
Timu ya TP Mobale vile vile ikajipatiya ushindi kwa mikwaju ya pelnati zidi ya Munyago FA ya Uvira mikwaju 4-3.
Munamo dakika 90′ za mchezo matokeo ilikuwa ya Sare ya 0-0 pande zote mbili, la Mobale litakuwa Timu ya kwanza ya Kamituga kuingiya kwenye raundi ya nanne Yani 1/8.kisha ushindi ambao wameupata.
Hii kipindi ya fainali Ndogo itakuwa imeendelea hii jumapili tariki 19 may kwenye uwanja wa concorde mtaani Kadutu, na mechi mbili zitakuwa kwenye mpango.
Pa saa 13h As Kasms ya Kamituga itaipokea FC Café du Congo ya Fizi.
Pa saa 15h FC Vijana prestige ya Fizi itakuwa ikimenyana na Ed Mbila ya Kamituga.
Patrigal Basimarha soka.