Ilikuwa kwenyi mechi ya juma la Saba iliyo endeshwa hii jumamosi tarehe 09 novemba kwenye uwanja wa Kadutu ambayo Bukavu dawa imeifunza kazi hii timu ya FC Céleste kutoka Mbaka.

Kisha kuwa teketeza vikali na kuwa laza kwa goli tatu bila jibu ( 3-0) inakuwa ni ushindi wa pili ambao Timu la OC Bukavu dawa hapa Nyumbani mjini Bukavu.

Kisha kupoteza mechi mbili mfululizo dhidi ya Dauphin ya goma na Daring klabu Motema pembe ya Kinshasa, Bukavu dawa imekuja na Hasira kubwa na haitaki Ku fanya ziaka na timu yeyote ile nakupitiya lengo ambayo wanayo kwenye hili mashindano ya kitaifa ya ILLICOCASH.

Tuseme kwamba goli za Bukavu dawa ziliweza kujazwa Na mchezaji Olivier Nshokano na Kamango Salimu

Mukipindi ya kwanza ilikuwa kwenye dakika 6′ Za mchezo kupitiya mkwaju wa chini siyo mbali na lango la Timu FC Céleste na Mara moja mchezaji Olivier akauweka nyavumuni, na mukipindi cha pili cha lala Salama huyo mchezaji Olivier akajaza goli la pili kisha kutelezeshe  mpira ndani ya lango la hatari la FC Celeste Ku dakika 56′ za mchezo.

Na mchezaji Kamango Salimu alikuja kuharibu timu ya FC Céleste kwaku funga Bao ya tatu mu dakika 67′ ushindi huo imepatiya timu ya Bukavu dawa ichukuwe na fasi ya pili kwenye Kundi la pili ikiwa na  11 pointi kwa mechi Saba ambayo imesha cheza tayari.

Patrigal Basimarha soka

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *