Ilikuwa kwenye mechi ya mashindano ya shirika la mpira la Bukavu EUFBUK Daraja yake ya kwanza iliyo endeshwa hii jumapili tarehe 29 septemba kwenye uwanja wa Kadutu.

 Ambapo hii timu ya Bilombe akaionesha timu ya Safari Nini ilicho itowa kanga manyoya kwa kuwazala kwa goli nne kwa moja, Bilombe iliweza kuipiga timu ya Safari ilikuwa mapema sana kisha mechi kuanza mudakika nne (4′) Walikuwa tayari walisha jaza goli mbili.

Ila timu la US Safari ikaweza kugombowa goli moja mnano dakika kumi nasita (16′) kupitiya mkwaju wa pelnati. ila Timu ya US Bilombe wachezaji wake hawakukata matumaini wanaendelea kushambulia timu ya Safari na wakabahatisha kujaza goli lao la tatu mu kipindi ya kwanza.

Nani matokeo hiyo iliweza kupeleka timu hizo mbili waende kwenye kipindi cha mapumziko ila Bilombe ilikuwa ikiongoza kwa mabao matatu kwa moja, walipo rudi kwenye kipindi ya pili ya lala Salama Timu ya Safari ikaweza kuanguka kifudifudi ndani ya Mikono ya Bilombe na kubanwa hadi njinsi wali weza kuwajaza goli ya inne.

Hizi goli za Timu ya Bilombe ziliweza kujazwa naye mshambuliaji machachari Yves Nyamukere goli ya kwanza na goli ya pili mu dakika nne( 4′) za mchezo 

Mubeki wa nyuma Wabi wakwinga akaweza kujaza goli la tatu mudakika ishirini (20′) za mchezo.

Na mchezaji Bruno Mutondo Ntonga akaweza kufunga goli ya nne kipindi ya Salama ilikuwa mudakika sabini n’a tano ama (75′) kupitiya chapisho nzuri yake mchezaji Mashahuri Yves Nyamukere, tuseme kwamba mchezaji Yves iliweza kuchaguliwa kama mchezaji bora wa hii mechi kupitiya shapisho mbili na goli ambayo aliweza kuzifunga kwa hii mechi.

Kupitiya ushindi hii timu ya Bilombe inaendelea kushikilia na fasi ya pili kwa muda katika kundi lake ikiwa na pointi 14 pts kwa mechi Sita.

Na Safari inaendelea kushikilia na fasi ya Saba kwa muda ikiwa na pointi 7 pts kwa mechi Sita, hii timu ya Safari haijawai shinda hata mechi moja uwanjani kwa hizo pointi 7 pts ambazo inayo iliwezaga kushinda Ciriri sport kwacha Ama forfait na kushinda vile vile FC Orgaman kwache kisha mechi ambayo iliwezaka maliza ya Sare ya bao mbili pande zote Ila Safari ikaweza kuishinda Orgaman sababu FC Orgaman ilikuwa bado haija lipa bima ama assurance.

Patrigal Basimarha soka.

 

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *