Mabingwa hao wa Kivu Kusini watasafiri kwa ndege saa 6:30 mchana hadi Kinshasa.

Kwajili ya kuwakilisha Jimbo la Kivu kusini kwa hii mashindano la wachezaji wachini ya miaka kumi na Saba umaarufu 17 ans, hawa mabingwa kwa mechi ambazo waliweza kuzicheza kwa hii mzunguko wa sita walicheza mechi Saba na Wakajipatiya ushindi kwa mechi sita na mechi Moja wakaenda Sare.

Hii timu imefanya vema zaidi kwenye mstari na kwenye njia ambayo waliweza Kupitiya hapa jimboni ikiwa ni mara ya kwanza timu hii inashiriki kwenye mashindano, itakuwa ikiwakilisha walaya ya Walungu na mkoa Kivu kusini yote mzima.

Ujumbe huu mkali unaundwa na watu 25 wakiwemo wachezaji 18, mshauri wa 1, mweka hazina, katibu, wanahabari wawili na rais wa ligi ya vijana ya Kivu Kusini.

kumbuka kuwa mabingwa wa Kivu Kusini u17 wamefuzu kwa michuano ya taifa ya vijana itakayoanza Agosti 3, 2024 na itasindikizwa na timu nyingine mbili kutoka SK ikiwemo Panzi United kutoka Bukavu, na TP Buloho kutoka Kahuzi Biega.

 Baudry Birego Albert  mwandishi wa habari za michezo, alikuwa akizungumza mbele ya Ripota wa Congoleo nakukamlisha habari hizi za Timu ya Kanga Suzuki motard.

Patrigal Basimarha soka

Laisser un commentaire

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *